HABARI zilizopatikana jioni hii zinasema kuwa Mwanamuziki mahiri wa Hip-Hop kutoka Tanzania, Albert Mangwair amefariki dunia huko nchini Afrika Kusini kwenye hospitali ya Hellena Joseph.
Aidha, taarifa kutoka kwa mmoja wa mtu wa karibu wa Ngwair nchini humo, Hussein Original aliyepo mji wa Pretoria, alisema alikutwa na umauti huo majira ya asubuhi, akiwa 'geto' na na msanii mwenzake ‘M To The P’. Inadaiwa walipoenda kuwagongea asubuhi, walikuta Ngwear amefariki na M To The P amepoteza fahamu.
Hata hivyo, Daktari tayari alishathibitisha taarifa hizo na tayari ametoa taarifa kwa watu wa karibu wa msani huyo.
Taarifa zaidi juu ya tukio hili tutaendelea kuwajuza kuhusiana na hali halisi
ya Ngwair aliyeanza kutamba na kibao cha Ghetho
langu na baadae wimbo wa Mikasi.
No comments:
Post a Comment