Tuesday 28 May 2013

HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA UZINDUZI WA SHINDANO LA BIG BROTHER THE CHASE

Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya kamera yetu.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.

Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg jana usiku. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

Mwakilishi kutoka Tanzania Ammy Nando akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show. Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.

Burudani zikiendelea.

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.

Mwakilishi wa Tanzania Feza Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.

Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi jana jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Feza Kessy mshiriki kutoka Tanzania.

Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo

BAADA YA KUNENEWA MENGI ADAM MCHOMVU KUUSU KAULI KUMCHAFUA JAYDEE HATIMAYE AMEAMUA KUFUNGUKA KAULI HII HAPA




Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu amejikuta kwenye wakati mgumu baada leo akaunti yake ya Facebook kuonesha imepost link yenye kichwa cha habari ‘Picha za uchi alizopiga Lady Jay D bofya hapa’. Kutokana na post hiyo, Adam amejikuta akitukanwa matusi mengi ya nguoni kitendo kilichomlazimu aombe radhi japo anadai hakuandika yeye.

“Naomba kuchukua nafasi hii kuomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa maneno machafu yaliyoandikwa kwa wall yangu, na pia naomba nieleweke kwamba sihusiki na chochote kupost au kuandika chochote kuhusu kikwete foundation na picha za jdee ukiwa naked, sina ugomvi na yeyote naheshimu hisia za kila mtu nikiamini kila mtu ana maamuzi yake.. Aliyeamua kutumia jina langu kufanya hayo najua sasa unajiskia vizuri baada ya matusi mengi niliyotukanwa.. Maisha hayaishii hapa siku zinaenda na ukwali utafahamika siku moja … Mchana mwema.”

“Mi namuachia Mungu … Ya duniani yatalipwa hapa hapa, anayetengeneza mazingira haya kunichafua ni baraka zinaongezeka .. I keep on moving sirusishwi nyuma na kauli zenu zilizojaa chuki, dharau maisha Yanaendelea.
Kiukweli napata lawama nyingi matusi mengi bila kujua kosa langu.. Account yangu ni hii sina nyingine na sijui nn kimeendelea huko, kiroho safi tu naomba mtu aniambie kuna nini wapi nijue ivi mtanilaumu bure tu.. No hard feelings.”

TAIFA STARS KUWASILI NCHINI ETHIOPIA NAKUANZA KUNOA MAKALI

kikosi cha timu ya tifa tanzania kikiwa na mwonekano mpya wa vazi la suti
Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech. Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0. Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi. Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech

MSANII WA KIZAZI KIPYA ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI



HABARI zilizopatikana jioni hii zinasema kuwa Mwanamuziki mahiri wa Hip-Hop kutoka Tanzania, Albert Mangwair amefariki dunia huko nchini Afrika Kusini kwenye hospitali ya Hellena Joseph.
Aidha, taarifa kutoka kwa mmoja wa mtu wa karibu wa Ngwair nchini humo, Hussein Original aliyepo mji wa Pretoria, alisema alikutwa na umauti huo majira ya asubuhi, akiwa 'geto' na na msanii mwenzake ‘M To The P’. Inadaiwa walipoenda kuwagongea asubuhi, walikuta Ngwear amefariki na M To The P amepoteza fahamu.
Hata hivyo, Daktari tayari alishathibitisha taarifa hizo na tayari ametoa taarifa kwa watu wa karibu wa msani huyo.
Taarifa zaidi juu ya tukio hili tutaendelea kuwajuza kuhusiana na hali halisi
ya Ngwair aliyeanza kutamba na kibao cha Ghetho
langu na baadae wimbo wa Mikasi.

TIMU YA ARSENAL HATARINI KUMKOSA JOVETIC




Mchezaji anayetakiwa kwa muda mrefu Arsenal, Stevan Jovetic wa Fiorentina anauzwa Pauni Milioni 25



Andrey Arshavin (kushoto), akiwa mazoezini na Jack Wilshere, anaweza kutimkia Zenit St Petersburg

MPANGO wa Arsenal kumsajili Stevan Jovetic uko hatarini kubuma kwa sababu zile zile mashuhuri za klabu hiyo ya London, 'ubakhili uliotukuka'.

Arsenal imeshindwa kutoa dau la Pauni Milioni 25 ambalo Fiorentina wanataka ili kumtoa Jovetic.

Mazungumzo baina ya klabu hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa, baada ya kocha Arsene Wenger kumfanya Jovetic mchezaji nambari moja katika orodha ya nyota anaowataka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.

Lakini mpango huo unaelekea kugonga mwamba kutokana na klabu hiyo ya Serie A kugoma kuchukua kiasi chochote cha fedha chini ya Pauni Milioni 25 walizotaka.

Mabosi wa Gunners, wameiambia Fiorentina wako tayari kulipa tu Pauni Milioni 20 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Montenegro na kuna wasiwasi Juventus nao wanamnyatia Jovetic.

Kama Arsenal, vigogo hao Italia nao wameanzisha mazungumzo na klabu yake juu ya kumsajili Jovetic — lakini inafahamika itakuwa jambo gumu kwa Fiorentina kuwauzia silaha
wapinzani wake.

Pamoja na hayo, Juventus wako tayari kutoa dau ambalo Fiorentina wanataka, ili kuwabadilisha mawazo yao.

Wakati huo huo, Andrey Arshavin, ambaye amemaliza mkataba wake, anatakiwa na Zenit St Petersburg. Mshika Bunduki huyo 'aliyetepeta', ambaye analipwa Pauni 90,000 kwa wiki, pia ana za kwenda kucheza Marekani na Mashariki ya Kat

DAVID VILLA KUTOLEWA PAUNI MILLIONI 10 NA SPURS




Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa anatakiwa Tottenham kwa Pauni Milioni 10

KLABU ya Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kwa Pauni Milioni 10, mshambuliaji wa Barcelona David Villa na pia wamefufua nia yao ya kumsajili mchezaji wanayemtaka kwa muda mrefu, Leandro Damiao.

Andre Villas-Boas aliibua nia ya kumsajili ya Villa mapema mwezi huu na sasa klabu yake nchini Hispania iko tayari kuisikiliza Spurs katika mpango wao wa kumnasa mkali huyo wa mabao kwa ajili ya msimu ujao.
Klabu hiyo ya Nou Camp iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye amejikuta katika wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza na anaweza akauzwa kwa Pauni Milioni 12. Chanzo Clan infos

Monday 27 May 2013

ANGALIA KATIKA BLOGU HII UMUONE MSHINDI WA THE MIC VODACOM KING 2013 WAKATI ANAKABIDHIWA GARI






CCM:IMEDHAMIRIA KUZOA KATA 25



CHAMA Cha Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika kata mbalimbali nchini.


Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo. Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na Zuberi Nyamoleo.


"Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;


"Pale Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".


Kinana aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na Nyamoleo kwa kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani katika kata ya Mbalamaziwa.


"Ninyi ni watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema Kinana.


Kinana alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.


"Mwanachama lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.


Kinana alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.


"Tafadhalini sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.


Kinana alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

WASANII WANAO JIHUSISHA NA MASWALA YA UCHORAJI WAKABIDHI PICHA YA RAIS JAKAYA KIKWETE


BAYERN WAKISHANGILIA UBINGWA LONDON,WAKIONGOZWA NA Heynckes na Scheinsteger

baye2 c4886
Kombe

baye3 1d79c

baye4 3c4e5

baye5 3e279
baye6 59c3a
baye7 78d6b
baye8 5cda3
baye c6eb8
Baada ya wekundu wa kusini mwa Ujerumani, `The Bavarian`, Bayern Munich na mabingwa wa Bundesliga msimu wa 2012/2013 kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya usiku wa kuamkia leo kwa kuwatandika Nyuki wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyi Borussia Dortmund mabao 2-1, wamepiga bonge la sherehe na kuwaacha Waingereza wakiduwaa katika ardhi yao.

Saturday 25 May 2013

KIVUMBI LEO WEMBLEY KATIKA FAINALI YA KOMBE MABINGWA ULAYA (UEFA)

 g 7f9c1

Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borrusia Dotmund
FAINALI ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali. Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.

Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya

RAIS WA ZANZIBER AMTEBELEA SHEHA ALIYE TIWA TINDIKALI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyetiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa pili kulia Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.

LADY JAY DEE AMSHANGAA MWANA FA KWA ALICHOKIFANYA: SOMA ALIICHOKISEMA






Kutokana na JIDE kuwa na show yake kubwa mnamo tarehe 31 mwezi huu pale nyumbani lounge ,Sasa rafikiye wa karibu sana MwanaFA inaonyesha naye ameanda show yake siku hiyohiyo  ya Tarehe 31,Zaidi ya yote mwana FA akawachukua  wasanii walio jitoa katika show ya JIDE kama Linnah  sa kutokana na sitofahamu hiyo mtandao huu wa thechoicetz uliweza kumtafuta JIDE kupitia twitter na kumuu liza juu ya hili swala naye aliweza kutoa yake anayo yafikiria,pia mtandao huu wa thechoicetz ulimtafuta  MwanaFA lakini mwanaFA hakuweza kutujibu swali tulilo muuliza hadi muda huu.

Friday 24 May 2013

Wasanii watakaotumbuiza kwenye show ya ufunguzi wa Big Brother Africa watajwa

Stella Mwangi
Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini.
Wande-Coal-Album
Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika nchi 50 barani Afrika. Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya Big Brother, www.bigbrotherafrica.com

Wednesday 22 May 2013

blog ipo kwnye matengenezo halaaa up coming blog clan infos

hi ma  people  this izy brand  new  blog    up coming  blog   ineed  your cooperation   at all   blog which  contain  story   music  and  gossipe  infos   call  clan infos  more than  up coming  blog  apps  as  crue  of clan infos  we love all who give  as  coperation