Sunday 23 June 2013

kocha wa arsenal ajitosa rasmi kumuwania mshambuliaji wa manchester united wayne rooney





Wayne Rooney



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
KLABU ya Arsenal baada ya kumalizana kwa dau la Pauni Milioni 22 na Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid, sasa inahamishia nguvu zake kwa mshambuliaji wa Manchester United, anayeuzwa Pauni Milioni 20, Wayne Rooney - huku kocha Arsene Wenger akiwa amedhamiria kuendelea kumtumia katika nafasi ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Muargentina huyo.

Higuain ni mchezaji ambaye Arsenal sasa wana uhakika wa kumnasa, huku Carlo Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao wa Hispania, akitarajiwa kutua leo kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.

Lakini katika uhamisho huo wa Rooney, Arsenal italazimika kumlipa mshahara wake wa Pauni 220,000 kwa wiki, ambao ni mkubwa mno kulingana na tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu 'bakhili'.
Wenger haoni kama Rooney ni mshambuliaji wa kati, lakini kama kiunganishi, baina ya kiungo na Higuain — nafasi ambayo mchezaji mwenyewe amesema inamfaa
Lakini Chelsea pia inamtaka Rooney na kocha mpya wa United, David Moyes anatarajiwa kukutana na Rooney wiki mbili zijazo, hivyo uwezekano wa yeye kujiunga na klabu hiyo ya London bado mdogo.
United haitataka kumuuza Rooney kwa Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa washindani wao wakuu katika mbio za ubingwa na matumaini ya mchezaji huyo yanabakia katika kikao chake na Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo mpya mzuri Old Trafford, hususan baada ya klabu kusema hajawahi kuomba kuondoka United.
Hilo ni suala lililotokana na wasiwasi wa Rooney juu ya uhusiano wake na mashabiki wa United. Rooney anatarajia kikao kama alichowahi kufanya na kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita, cha binafasi kujadili mustakabali wake katika klabu. Arsenal imetenga bajeti ya kutosha kupambana katoka soko la usajili, lakini tatizo ni kwamba wataweza kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa sababu ni wenye kiu ya mataji, vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo vimekuwa adimu

Brazil yaitwanga 2-1 Italia, zatinga nusu fainali kombe la mabara




Neyman akishangilia bao



Neyman akifunga bao







Javier Hernandez amefunga mawili dhidi ya Japan

MABAO ya Dante dakika ya 45, Neymar 55 na mawili ya Fred dakika za 66 na 88 yameipa Brazil ushindi waliostahili wa 4-2 dhidi a Italia usiku wa kuamkia leo na kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mabara ikishinda mechi zote katika Kundi A.

Italia ilipata mabao yake kupitia kwa Giaccherini dakika ya 51 na Chiellini dakika ya 71.

Kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz/Dante dk33, Marcelo, Gustavo, Hernanes, Hulk/Fernando dk76, Oscar, Neymar/Bernard dk68 na Fred.

Italia: Buffon, Abate/Maggio dk30, Bonucci, De Sciglio, Chiellini, Candreva, Aquilani, Marchisio, Montolivo/Giaccherini dk26, Diamanti/El Shaarawy dk71 na Balotelli.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Javier Hernandez alifunga mabao mawli na kukosa penalti Mexico ikiifunga Japan 2-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A. Bao la Japan lilifungwa na Shinji Okazaki na sasa Brazil inaungana na Italia kusonga Nusu Fainali.

Saturday 22 June 2013

IMEVUJA, MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA





TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa

HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA SHOW YA MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGA(NEW MSASANI DSM)



Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam.

Chid Benz
Fukuda akichana mistari

Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.


Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi.
Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.


Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza





Afande Sele akipagawisha mashabiki.

MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA CROATIA AFARIKI DUNIA UWANJANI



Alen Pamic aliyelala, akipatiwa huduma ya kwanza na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni kutokana na matatizo ya moyo.
ALEN PAMIC

ZAGREB, Croatia
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo
NYOTA wa soka la kulipwa raia wa Croatia, Alen Pamic ameanguka uwanjani na kufariki dunia wakati wa mechi ndogo isiyo ya kimashindano, gazeti la kila siku la Vecernji List limesema katika toleo lake mtandaoni la leo Jumamosi.
Taarifa hiyo imeripotiwa kwa ufupi, huku ikiwa haina maelezo zaidi kuhusiana na kifo cha Pamic aliyekufa akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic, aliyekuwa akichezea klabu ya NK Istra 1961 katika ligi ya daraja la juu zaidi nchini hapa, alikuwa na historia ya matatizo ya moyo, ambayo yalimwangusha dimbani mara tatu kabla ya tukio hilo lililochukua uhai wake.
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo.
Pamic aliyekuwa kiungo mahiri dimbani, aliutumia msimu mmoja wa 2010/11 kuchezea klabu ya Standard Liege ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, lakini klabu hiyo ikamtema muda mfupi baada ya kupata shambulio la moyo na kuzimia akiwa mazoezini, gazeti la Vecernji limesema katika taarifa yake.
Pamic ni mtoto wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Croatia, Igor Pamic, ambaye kwa sasa anainoa klabu ya NK Istra 1961 aliyokuwa akiichezea marehemu

HUU NDIO UJIO MPYA WA AMINI

AMINI

BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Ni wewe’, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’ anajipanga kuachia video ya kibao chake cha ‘Sipo nae’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaama, Amini alisema anamshukuru mungu kazi hiyo imefanya vizuri na anaamini itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya kibao hicho.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika studio ijulikanayo kwa jina la Shany chini ya mtengenezaji mahiri Mr. T ambaye anauhakika amemtendea haki katika kazi hiyo.
“Mtayarishaji wangu namuamini sana, hivyo najua wadau wengine wataupenda wimbo kulingana na vionjo ambavyo amevitumia mbali na ujumbe uliopo katika kazi hiyo.” alisema Amini.
Pia aliwaomba wadau na mashabiki wa muziki nchini kumpa sapoti katika kazi zake na wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Amini alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Robo saa’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga

ROONEY KUVUTWA SHATI KATIKA TIMU YA REAL MADRID

WYNE ROONEY



KOCHA mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atafanya harakati za kumsajili Wayne Rooney majira haya ya joto kama mshambuliaji huyo asiye na furaha atashindwa kumaliza tofauti zake na Manchester United.

Rooney anapenda zaidi kuungana na Jose Mourinho pale Chelsea ikiwa atamaliza miaka yake tisa ya kuishi United, lakini Madrid itakuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa ataondoka.

Klabu zote zina uwezo sana tu wa kulipa Pauni Milioni 30 za ada ya uhamisho wake na kumlipa mchezaji mwenyewe mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Ancelotti anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho Jumatatu na atakabidhiwa orodha ya wachezaji wanaotakiwa, wakiwemo Rooney, Gareth Bale, Edinson Cavani na Luis Suarez. Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake, atakuwa na mazungumzo na kocha mpya wa United, David Moyes baada ya wote kurejea kutoka mapumziko

HII HAPA HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA LA(1)





FUFA WORLD CUP HISTORY



WAKATI vugugu la kuelekea kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil likipamba moto, ni vema

tukaipitia historia ya mchezo wa kandanda ili, kwetu wapenzi wa mchezo huo, kujikumbusha historia yake.

Naam, mchezo wa kandanda una historia ndefu. Mwaka 1863 ndipo pale kandanda ya mpangilio ilipoona mwanga wa dunia. Hii ni baada ya nchi ya Uingereza kuutengenezea
mchezo huo sheria , kanuni na taratibu za kuucheza. Kabla ya hapo, kandanda
ulikuwa ni mchezo uliochezwa bila mpangilio maalum. Kulikuwa hakuna
sheria wala kanuni zilizowekwa juu ya mchezo huo.

Ni kwa sababu hii, Uingereza hadi leo hii inajiona kuwa ni “Mama wa Kandanda”. Matukio kadhaa ya


kihistoria ya mchezo huo yameonyesha ni jinsi gani Uingereza , kwa kujiona kuwa wao ndio waanzilishi wa kandanda duniani, wamekuwa wakionyesha majigambo ya wazi na wakati mwingine kuzuia kwa makusudi juhudi za wengine katika kufikiri namna nzuri ya kuuendeleza mchezo huo, mchezo ambao Waingereza wanaamini kuwa ni wao.

Hakuna ajabu baada ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mara ya kwanza mwaka 1966,
Uingereza ilionyesha azma yake ya kuandaa fainali za mchezo huo
kwa mwaka 2018. Hata hivyo, Qatar ndio iliyopata bahati hiyo.

Ikumbukwe, kuwa mwaka 2012 Uingereza iliandaa michezo ya
olimpiki kwa mataifa ya dunia. Kama wangepewa nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia miaka sita baada ya 2012, yaani, 2018, basi, Waingereza wangependa waitangaze nchi yao, kama taifa ambalo, katika kipindi cha mwongo mmoja ( miaka kumi) limeweza kupata
mafanikio makubwa na ya kihistoria ya kimichezo kwa kuwa mwenyeji wa matukio
makubwa mawili ya kimichezo duniani; Olimpiki na Fainali za Kombe la Dunia.
Kwamba Uingereza ni taifa kubwa.

Siku zote, Uingereza inajivunia historia ya kandanda kuwa upande wao. Itakumbukwa, kuwa ilikuwa ni mwezi Oktoba ya tarehe 26 mwaka 1863 pale shirikisho la kandanda nchini Uingereza (FA) lilipoanzishwa rasmi jijini London. Miaka 17 iliyofuata hata Scotland, Wales. Ireland nazo zikaanzisha mashirikisho yao ya soka.

Denmark ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Uingereza kuanzisha shirikisho lake la soka. Ilikuwa ni mwaka 1889. Lakini FIFA, shirikisho la soka duniani lilipoanzishwa rasmi mwaka 1904, liliundwa bila kuishirikisha Uingereza. Hii ilitokana na Uingereza kutokutuma mwakilishi wake kwenye majadiliano ya kuanzishwa kwa FIFA.

Kilichopelekea hilo ni dharu ya Waingereza ambao waliamini, kuwa
FIFA haikiuwa na lolote la kuchangia katika soka ukiondoa Waingereza wenyewe
walioasisi mchezo huo. Kwa namna fulani, ni hapa tunaweza pia kuyaona majigambo ya Waingereza katika kandanda.

Kwa vile Uingereza inaundwa na visiwa, kuna utani, kuwa hii ni hulka ya watu
waishio visiwani; kuwa hawaoni kingine mbali ya maji yaliyo mbele yao,
hujiona kuwa wao ni kila kitu.Uingereza waliendelea kuigomea FIFA na kutojihusisha nayo hadi mwaka 1924.


Nchi zilizotuma wajumbe waliohusika na kuunda FIFA ni kama zifuatazo;
Ubelgiji, Ufaransa, Hispania, Uholanzi, Denmark na Sweden. Vinara
waliopelekea kuundwa kwa FIFA ni matajiri wawili wakubwa kwa wakati huo;
Mholanzi Hirschman na Mfaransa Robert Guerin.

Kitendo cha Uingereza cha kujitazama yenyewe tu na kuibuka kwa
Vita Kuu Ya Kwanza ya Dunia kulipelekea mipango ya FIFA kuanzisha michezo ya
Kombe La Dunia kwa mara ya kwanza kuahirishwa na kusogezwa mbele. Na hata
vita vilipomalizika, Uingereza ilikataa katakata kuruhusu timu yake ya taifa
pamoja na washirika wao katika vita kukutana na kucheza na timu za mataifa
yaliyokuwa adui zao katika vita.

Hata hivyo, pamoja na Uingereza kujiunga na FIFA mwaka 1924, bado katika Fainali za kwanza za Kombe la Dunia zilizoandaliwa na FIFA mwaka 1930, Uingereza haikushiriki. Walisusa tena.

Je, ni kwanini Waingereza walisusa kucheza fainali za kwanza za
Kombe la Dunia? Je, jeuri na majigambo haya ya Waingereza ni sawa na mbio za
sakafuni ambazo huishia ukutani? Ni nini ilikuwa hatma ya msuguano huu kati
ya FIFA na Waingereza? Endelea kufuatilia simulizi hii ya kombe la dunia

0752887944 mwendaa lucas



Friday 14 June 2013

Bajeti : Ushuru wapiga hodi kwa watumiaji fedha kwa simu,ahueni kwa wamiliki wa bodaboda

 Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akiingia bungeni Dodoma jana kusoma hotuba ya Bajeti. Picha na Fidelis Felix
Dar na Dodoma:  
Serikali jana ilitangaza Bajeti yake kuu kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambayo inaashiria machungu kutokana na ongezeko la kodi na ushuru katika baadhi ya bidhaa, zikiwamo mafuta, soda, vinywaji vikali pamoja na leseni za magari.

Akisoma bajeti hiyo bungeni jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa pia alitangaza kuanzisha kodi na ushuru katika huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia simu za mkononi, ikiwamo kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha.

“Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 14.5 kwenye huduma zote (all mobile phone services) za simu za kiganjani/mkononi badala ya muda wa maongezi tu (airtime alone),” alisema Dk Mgimwa na kuongeza: “Katika ushuru huu, asilimia 2.5 zitatumika kugharimia elimu nchini.”
Kutokana na hali hiyo, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk Oswald Mashindano amelaumu kile alichokiita kuwa ukubwa wa kodi hasa kwa wasio na kipato kikubwa ili kufidia uendeshaji wa Serikali.

“Kama kawaida kutakuwa na ongezeko la mapato ya Serikali kutoka katika vyanzo vyake hasa ukusanyaji wa kodi. Inamaanisha kuwa kutakuwa na mzigo mkubwa kwa walipakodi hasa kundi la wenye kipato kidogo.

“Tofauti na nchi zilizoendelea ambazo wenye mitaji mikubwa ndiyo wanaobanwa kulipa kodi zaidi, nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwamo, kuna udhaifu mkubwa wa kukusanya kodi,” alisema Dk Mashindano.
Mafuta na magari

Waziri Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itapandisha ushuru wa mafuta ya dizeli kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 kwa lita, likiwa ni ongezeko la shilingi 2.

“Tumeongeza Sh2 tu kwa kuwa tunatambua tukiongeza ushuru mkubwa kwa magari makubwa ambayo yanatoa huduma kwa jamii, tutawaumiza wananchi,” alisema Dk Mgimwa.

Kadhalika, ushuru wa mafuta ya petroli umeongezwa kwa Sh61, kutoka Sh339 kwa lita hadi Sh400. Hata hivyo, imeongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa lita, sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita na wakati huohuo mafuta hayo yakiongezewa Sh50 kwa kila lita, fedha zitakazotumika kuchangia mfuko wa kusambaza umeme vijijini.

Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), umeongezewa kiasi cha Sh186.9 bilioni ambazo awali, hazikuwa zimetengwa baada ya Serikali kukubaliana na mapendekezo ya Bunge kupitia Kamati yake ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Serikali pia imepandisha viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari. Magari yenye ujazo wa injini yenye ukubwa wa kati ya cc 501 na 1500 yatatozwa Sh150,000 kutoka Sh100,000 za sasa.
Magari yenye ujazo wa cc 1501 hadi  2500 kiwango chake kimeongezeka kutoka Sh150,000 hadi Sh200,000 wakati magari yenye ujazo wa injini zaidi ya cc 2501 yatatozwa Sh250,000 kutoka kiwango cha sasa ambacho ni Sh200,000.

Hata hivyo, uamuzi huo hautazigusa bajaji na pikipiki (maarufu kama bodaboda) kwani Dk Mgimwa alisema vyombo ambavyo injini zake zina ujazo chini ya cc 501, ambavyo havitatozwa ada ya leseni. Ushuru pia umeongezwa kwenye magari yasiyokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25. Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari  chakavu  ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.

Pombe na Sigara

Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali na sigara. Vimeongezwa kodi kwa asilimia 10.
Ongezeko la kodi kwa kipimo cha lita moja ni kwa vinywaji vikali ambayo imepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631, sawa na ongezeko la Sh239, bia inayotengenezwa kwa nafaka za nchini ambayo haijaoteshwa, imepanda kutoka Sh310 hadi Sh341, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita wakati bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 hadi Sh578 sawa na ongezeko la Sh51.

Vinywaji baridi vimepanda kutoka Sh83 kwa lita hadi Sh91 sawa na ongezeko la Sh8 kwa lita.

Sigara zenye kichungi na zinazozalishwa nchini zimepanda kwa asilimia 75, kutoka Sh19,410 hadi Sh21, 351 kwa sigara 1,000 sawa na ongezeko la Sh1.94 na senti 94 kwa sigara moja.
Mabadiliko ya Sheria

Ili kutekeleza uamuzi wa kuongeza ushuru na kodi, Dk Mgimwa amependekeza kufanya maboresho ya sheria mbalimbali za kodi ambazo ni za; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Kodi ya Mapato, Ushuru wa Bidhaa, Ushuru wa Mafuta, Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Sheria ya Usalama Barabarani. Nyingine ni Sheria za; Petroli (Petroleum Act), Uwekezaji Tanzania, Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na marekebisho mengine madogomadogo katika baadhi ya sheria za kodi.

Dk Mgimwa alisema mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji yanalenga kutoza asilimia 25 ya ushuru wa forodha unaopaswa kutozwa kwenye bidhaa zinazotambulika kama “Deemed Capital Goods” (yaani kutoa msamaha wa kodi wa asilimia 75 kwenye bidhaa hizo badala ya asilimia 90 za sasa) na kuondoa baadhi ya bidhaa kwenye orodha ya kupata msamaha.

“Bidhaa hizo ni zile ambazo hazina uasilia wa kuwa bidhaa za mtaji kama vile vifaa vya ofisi, samani, sukari, vinywaji (viburudisho), bidhaa za mafuta ya petroli, magari madogo (Non Utility Motor Vehicles), viyoyozi, majokofu, na vifaa vya kielektroniki, mashuka, vijiko, vikombe nk,” alisema waziri huyo. Alisema marekebisho hayo pia yanalenga kupunguza misamaha ya kodi na kubakiza misamaha yenye tija na yenye kuchochea uwekezaji mkubwa katika sekta za uchumi za kimkakati, hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Alisema pato la taifa linatarajiwa kukua kutoka asilimia 7.0 mwaka 2013 hadi asilimia 7.2 mwaka 2014 na wakati huohuo, bei zikitarajiwa kubaki kwenye viwango vya tarakimu moja na mfumuko wa bei kushuka hadi asilimia 6.0 Juni 2014.
Kuhusu akiba ya fedha za kigeni, Dk Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali itajitahidi kuwa na akiba itakayoweza kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Alisema jitihada zitafanywa ili kupunguza tofauti ya viwango vya riba vya kuweka na kukopa na kuimarisha thamani ya shilingi na kuwa na kiwango imara cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

Mbowe, wabunge

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe alisema: “Bajeti ya mwaka huu haina jipya” kwani Serikali imeendelea kupandisha kodi katika bidhaa zilizozoeleka badala ya kusimamia kodi kwenye rasilimali za nchi.
“Bajeti hii inaonyesha Serikali ilivyokosa ubunifu wa vyanzo vya mapato, kila mwaka wanapandisha kodi kwenye bia, sigara, magari na mafuta,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia alisema sheria ya ununuzi ikirekebishwa kama alivyoahidi Waziri Mgimwa itasaidia kupunguza gharama ya bidhaa mbalimbali.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema kuongezwa kwa fedha za mfuko wa vijana ni ukombozi kwa kuwa miaka mingi kilio hicho hakikusikika.

“Tunaona sasa Serikali imekuwa sikivu kwa kuwa kwa muda mrefu tuliomba lakini hatukupewa,” alisema baada ya Serikali kuongeza Sh3 bilioni kwa ajili ya mfuko

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF



TIKETI MECHI YA STARS KUANZA KUUZWA LEO JUNI 14.
Wakati timu ya Ivory Coast inatarajiwa kuwasili leo usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, tiketi kwa ajili ya mechi kati yake na Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa zinaanza kuuzwa kesho mchana (Juni 14 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Vituo vitakavyotumika kwa mauzo hayo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani. Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, sh. 7,000 viti vya rangi ya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000. Pia viti 100 vilivyo katika sehemu ya Wageni Maalumu (VVIP) vitauzwa kwa sh. 50,000 kila kimoja. Tiketi hizo zitauzwa katika ofisi za TFF, na watakaonunua watapewa kadi maalumu zenye majina yao, majina ambayo pia watayakuta katika vita watakavyokaa. Kwa maana hiyo hakutakuwa pasi maalumu (free pass) za kuingia VIP.


PONGEZI KWA RAIS MPYA WA ZFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza Rais mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina aliyechaguliwa katika uchaguzo mdogo uliofanyika hivi karibuni. Amesema ushindi aliopata Faina unaonyesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA walivyo na imani naye katika kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu visiwani humo. Rais Tenga amesema ni imani yake kuwa Rais Faina ataendeleza ushirikiano uliopo kati ya TFF na ZFA kwa ajili ya ustawi wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumtakiwa kila kheri katika wadhifa wake huo mpya.



WAAMUZI WATATU WAFUNGIWA MIEZI MITATU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungia miezi mitatu waamuzi watatu walioshindwa kuchezesha mechi namba 32 ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Mpwapwa Stars ya Dodoma na Machava FC ya Kilimanjaro iliyokuwa ichezwe Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. TFF kupitia Kamati yake ya Waamuzi iliyokutana katika kikao chake cha Juni 12 mwaka huu kupitia taarifa mbalimbali za waamuzi wa RCL ilibaini makosa yaliyofanywa na baadhi ya waamuzi na kuyatolea uamuzi. Waamuzi hao waliofungiwa ambao wanatoka mkoani Singida ni Jilili Abdallah, Amani Mwaipaja na Theofil Tegamisho. Wamefungiwa kwa kutoripoti katika kituo walichopangiwa (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma) na kutoa taarifa ya uongo kwa kushirikiana na Kamishna wa mechi hiyo. Kanuni iliyotumika kuwafungia ni ya 28 kifungu (d) na (g) ya Ligi za TFF, na adhabu hiyo imeanza Juni 13 mwaka huu. Waamuzi hao pamoja na kamishna badala ya kwenda Uwanja wa Jamhuri, wao walikwenda kwenye Uwanja wa Mgambo ulioko Mpwapwa na kuandika ripoti iliyoonesha kuwa timu ya Machava FC haikufika uwanjani wakati wakijua kuwa mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri

MAKALA KUSU USIKU WA TUZO ZA 'KTMA 2013 - KIKWETU KWETU'



Mshindi wa tuzo tatu za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013, Kala Jeremiah (katikati) akitoa neno la shukrani. Kushoto ni Mtayarishaji D Classic aliyefanya wimbo Dear God uliompa Jeremiah tuzo hizo.

Mwanamuzi Hussein Jumbe, akichana mistari ya kibao cha Khaleed Mohammed 'TID' kiitwacho Zeze katika usiku huo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.

Mkongwe Zahir Ali Zorro akikitendea haki kibao cha mkali wa Takeu, Lucas Mkenda kiitwacho Kikulacho.

Ommy Dimpoz kulia akipokea kutoka kwa msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, tuzo ya Wimbo Bora wa Kushikiana uitwao Me and You aliomshirikisha Vanessa Mdee (katikati).
DAR ES SALAAM, Tanzania
KI-KWETU Kwetu ilikuwa ndio kaulimbiu iliyobeba mchakato wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (Kilimanjaro Tanzania Music Awards – KTMA 2013), zilizofikia tamati Juni 8, katika Usiku wa Tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Hali ya mambo ilikuwa ya kuvutia mno katika usiku ule uliotanguliwa na kimya cha dakika moja kuomboleza kifo cha Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini na kuzikwa Juni 6, katika makaburi ya Kanisa la Mtakatifu Monica, Kihonda mjini Morogoro.
Burudani kali iliupamba usiku ule, huku mambo yakinoga kila dakika zilivyokuwa zikiyoyoma; kabla, wakati na hata baada ya tuzo hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager ‘Bonge la Kiburudisho.’
Waliohudhuria ‘Usiku wa Tuzo’ Mlimani City Jumamosi ile, watakuwa mashahidi wa hili na kwa kutambua thamani ya kilichofanywa na waratibu na wadhamini wakuu Kilimanjaro, nathubutu kusema; Hongera TBL, lakini pia kwa Basata na Innovex kwa kufanikisha mchakato.
Hongera kwa kufanikisha mchakato mzima wa KTMA 2013, ulioambatana na tuzo mili za ‘All of Fame’ iliyoenda kwa Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje na ile ya ‘Individual All of Fame’ iliyoenda kwa nyota wa zamani wa bendi ya Cuban Marimba, marehemu Salum Abdallah.
Hapa tunakuletea kwa ufupi matukio muhimu katika ‘Usiku wa Tuzo,’ ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa wa aina yake kwa wasanii Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz na Chalz Baba na Bendi yake ya Mashujaa kwa kutwaa tuzo nyingi kati ya tuzo 37 zilizotolewa.
Kala Jeremiah, Dimpoz, Mashujaa wang’ara KTMA

Kama ni utabiri uliotimia, gazeti hili linaweza kujivunia kuwatabiria vema wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz, ambao kupitia moja ya makala zake iliwataja kuwa ni wasanii walio kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na tuzo nyingi na kujiwekea rekodi. Usiku wa Tuzo KTMA 2013 ukathibitisha hilo kwa wakali hao kushinda tuzo tatu kila mmoja.

Kala Jeremiah alikuwa na usiku wa aina yake, ambapo alikuwa karibu atwae tuzo nne, ingawa aliishia kutwaa tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ile ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop (Dear God) iliyoenda kwa Nay wa Mitego kupitia wimbo Nasema Nao.

Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo nyingi zaidi (saba) katika kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You aliomshirikisha Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano.

Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae, huku akichemka katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume wa Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi wa Bongo Flava.

Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.

Pia nyota wake Fagasoni aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi. Ndo kusema Mashujaa wakiongozwa na Chalz Baba, ‘walitisha mno’ usiku ule na kuzipoteza bendi na wanamuziki mahiri wa dansi nchin
Dimpoz na ushindi wa ‘neno bora’ la ‘Usiku wa Tuzo’

Kwangu mimi, msanii Ommy Dimpoz alikuwa zaidi ya mshindi, kwani licha ya tuzo zake tatu, aliibuka mshindi pia kwa kutoa kauli nayoweza kuiita ‘bora zaidi’ kuliko zote zilizotolewa na washiriki wengine zaidi ya 100 waliofika ama kutuma wawakilishi wao.

Nyuma ya ‘neno bora,’ Dimpoz aliitoa tuzo moja kwa Vanessa Mdee, kati ya mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha ‘Me and You’ na kutafsiriwa kama ‘aliyempoza’ binti huyo aliyebwagwa katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe.

“Napenda kumshukuru kila aliyefanikisha mimi kupata tuzo hii, ambayo nina furaha kwani nimekabidhiwa tuzo hiyo shemeji yangu (akimaanisha Wema Sepetu aliyemkabidhi),” alisema Dimpoz huku akimtania; ‘Kama vipi tukutane baadaye shemeji.’

Akionekana kuiva na semina elekezi kwa wateule ‘nominees’ iliyotolewa na TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro, Dimpoz alisema: “Kama msanii na Mtanzania, napenda kusema kuwa, tumechoka kuwazika wasanii maskini wenye majina makubwa katika ‘game.’

“Ifike kipindi kila mmoja kwa nafasi yake aumizwe na hali duni kimaisha na kimapato tuliyonayo wasanii na kuzikwa tukiwa maskini licha ya majina makubwa tuliyonayo na kuyapata katika tasnia hii wakati wa uhai wetu,” alisisitiza Dimpoz huku akiamsha hisia za mashabiki ukumbini.

Ni kauli ambayo haiitaji ufafanuzi, ingawa mwenyewe hakusita kuifafanua: “Serikali na wadau wa muziki nchini, ndio wawezeshaji watakaofanikisha ukubwa wa majina yetu kwenda sambamba na pato letu.

“Serikali itusaidie kupitia michakato sahihi ya hatimiliki na wadau watoe kipaumbele kwa wasanii wa nyumbani. Sio tunafanya tamasha, huku maonesho yetu yakipambwa na picha za kina Messi (Lionel), kama wao ni zaidi yetu, basi waitwe tuone kama watashangiliwa,” alisema.

Dimpoz akawa ametoa ujumbe bora ambao kwangu mimi naupa ushindi wa ‘Neno Bora Zaidi’ la Usiku wa Tuzo, ambalo ni aghalabu kusikia likitamkwa na msanii, badala yake tungetegemea kulipata kutoka kwa Mgeni Rasmi, ambaye KTMA umfanya kuwa ni ‘Brand Manager’ na usiku ule alikuwa ni George Kavishe, Meneja wa Bia ya Safari.

Hussein Jumbe, Zahir Ali ‘Zorro’ Jose Mara wafunika

Burudani ukumbini zilianza saa 3:30 usiku kwa Mrisho Mpoto na wakali wanaounda Mjomba Bendi, waliopanda jukwaani baada ya dakika moja ya maombolezo ya kifo cha Ngwea – ambaye picha za msanii zilioneshwa katika kila ‘screen’ iliyokuwa ukumbini hapo.

Ahadi ya burudani kali kwa watakaohudhuria ‘Usiku wa Tuzo’ iliyotolewa na Kavishe ikaanza kudhihiri wasanii waliotumbuiza walipokuwa jukwaani. Amini Mwinyimkuu ‘Amini’ alifuata ‘Kikwetu Kwetu’ akiuchanganya wimbo wake wa Ni Wewe na ngoma ya Kabila la Wamakonde ‘Sindimba.’

Mtangazaji na Mtayarishaji wa Kipindi cha Supa Mix cha East African Radio na Uswazi cha East African TV, Hillary Daudi ‘Zembwela,’ akafuata mara kadhaa jukwaani na visa vilivyovunja mbavu vya Bure Mbaya kilichohusisha Dereva wa gari ya vichaa na kile cha Busara Haiuzwi kilichohusisha muuza mahindi mwenye kigugumizi.

Licha ya Zembwela kufunika na simulizi ya visa hivyo na vingine kibao, bado mashabiki hawatowasahau wakali wa muziki nchini Hussein Jumbe na Zahir Ali ‘Zorro,’ waliowapagawisha kwa aina ya muziki usio wao na nyimbo zisizokuwa zao pia huku wakizitendea haki.

Zilikuwa dakika 10 za kukata na shoka, ambapo Jumbe aliingia ukumbini saa 5:32 na kibao cha Zeze kilichoimbwa na Khaleed Mohammed TID. Zeze la Jumbe likaacha gumzo ukumbini, huku nyota huyo wa dansi akikitendea haki stejini kwa kukicheza na kunata na mistari.

Katika staili ya bandika-bandua ‘non-stop,’ saa 5:37, Jumbe akampisha Zorro aliyepanda na kibao cha Kikulacho kinguoni mwako, kilichoimbwa na mkali wa TAKEU, Lucas Mkenda ‘Mr Nice.’ Manjonjo ya Zorro wakawakumbusha wengi zama za Mr Nice. Hakika Zorro na Jumbe wakaacha midomo wazi mashabiki.

Mfululizo huo wa burudani za bandika bandua, ukaendelea saa 6:22, ambapo Barnabas Elias ‘Barnaba’ na Snura ‘Mama Majanga’ walifululiza kwa burudani kali, kisha kupisha tuzo kadhaa, kabla ya saa 6:55 mizuka ya wengi ukumbini kupandishwa tena na Jose Mara.

Jose mmoja wa nyota wanaounda kundi la Mapache Watatu, alijikusanyia fedha nyingi zaidi za kutuzwa jukwaani, ‘alipowakimbiza’ mashabiki kupitia kibao cha ‘Kinyaunyau’ cha Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje,’ na kufanya mfuko wa shati lake la Kinigeria kujaa noti na nyingine kumwagwa chini.

Lady Jaydee, Diamond wazua manung’uniko

Kama inavyoaminika, hakuna zuri lisilo na kasoro; Usiku wa Tuzo pia ulithibitisha kauli hii ya wahenga, ambapo baadhi ya mashabiki nje ya ukumbi katika ‘Red Carpet’ na hata ukumbini walionekana kukwazwa na kukosekana kwa wakali kadhaa wa muziki wakiwamo Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Judith Wambura ‘Lady Jaydee.’

Diamond Platnumz, aliyeibuka mshindi wa medali mbili za Msanii Bora wa Kiume na ile ya Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Flava, haikuelezwa nini kilisababisha kutofika ukumbini, ambapo tuzo zake hizo zilipokelewa kwa niaba yake na binti ambaye hata hivyo hakujitambulisha ni nani.

Hamu ya mashabiki kumuona Diamond iliyoanzia katika ‘Red Carpet’ ikaamshwa upya kila alipotajwa kushinda tuzo na kuzua maswali miongoni mwa mashabiki wake, kama ilivyokuwa pia kwa ‘swahiba’ wake wa siku za karibuni, Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Ney wa Mitego.

Ilikuwa hivyo kwa Jaydee. Mrembo wa Tanzania 2012, Brigite Alfred ndiye aliyepanda jukwaani kumtangaza mshindi wa kategori ya Msanii Bora wa Kike, ambapo Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Mwasiti Almasi na Recho walikuwa wakichuana.

Brigite akashika karatasi yenye jina la mshindi aliyoitoa katika bahasha na aliposema: Mshindi wa Msanii Bora wa Kike niii…..mashabiki wakalipuka kwa kelele ukumbini na kumalizia Lady Jaydeeeeeee!!!! Na wakarudia jina hilo mara kadhaa, kuionesha kukosa kwake mpinzani.

Ndipo aliposoma kwa kutaja jina la Jaydee kuwa mshindi na kuamsha shangwe ukumbini, iliyokuja kusindikizwa na maneno; shemejiii, shemejiiii, kufuatia mume wa Jaydee, Gadna G. Habashi kupanda jukwaani kumpokelea tuzo hiyo ya kategori pekee kwa nyota huyo mwaka huu.

Licha ya utetezi wa Gadna kuwa Jaydee yu safarini mkoani Shinyanga alikoenda kutumbuiza katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa mkoa huo, bado kiu ya mashabiki hao haikuweza kukatwa.

Ndipo Gadna alipowaamsha upya mashabiki hao alipowapa ujumbe wa nyota huyo wa kuwakaribisha katika tamasha la Juni 14 la kuadhimisha Miaka 13 ya Jaydee katika muziki, litakalofanyika kwenye Ukumbi wake wa Nyumbani Lounge, ambapo waliitikia: Tutakujaaaaaaaaa!!!!

Kauli ya mama wa Sharo Milionea/Ahadi za washindi

Kama ilivyotarajiwa, washindi wa tuzo mbalimbali walikuwa na kauli tofauti, zilizotanguliwa na ile ya Mama wa aliyekuwa mkali wa maigizo na muziki wa Bongo Flava, Ramadhani Mkieti ‘Sharo Milionea,’ Zaina Mkieti, aliyekuwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City kumwakilisha mwanaye aliyekuwa akiwania tuzo mbili.


Sharo Milionea alikuwa akiwania tuzo za Wimbo Bora wa Bongo Pop na Wimbo Bora wa Kushirikiana kupitia Chuki ni Bure aliomshirikisha Dully Sykess na akiwa katika ‘Red Carpet,’ Zaina akafunguka kuhusu tuzo hizo na namna anavyojisikia miezi sita tangu kifo cha mwanaye.

“Nashukuru kwa yote, michakato iliyofanikisha mimi kuwa hapa leo, lakini pia mwanangu kuwa mteule ‘nominees’ bila kujali kama atashinda ama atashindwa. Miezi sita sasa tangu kufariki kwa mwanangu, tukio hili linanipa faraja kuona kuwa Watanzania bado wanathamini kazi za marehemu mwanangu,” alisema Zaina.

Pia mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Citizen cha nchini Uganda (ambaye jina lake halikupatikana), aliyepokea tuzo Jose Chameleon, aliyeshinda kategori ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki, kupitia kibao cha Valu Valu, alikuwa na machache kuhusu muziki Afrika Mashariki.

Mtangazaji huyo alitoa ujumbe wa Chameleon kwa Watanzania, akiwataka wasanii na mashabiki wake kutoachwa nyuma na michakato mbalimbali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, badala yake wajiunge ili kupaa pamoja kimuziki nje ya ukanda huo unaojumuisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

“Ahsante Mungu kwa kunipa tuzo nyingine, ingawa hii nayo haitokani na wimbo mwingine, nakuomba wewe unijalie kazi nyingine, itakayoweza kutisha na kutwaa tuzo za mwaka mwingine,” alishukuru na kuahidi Kala Jeremiah akiigizia kibao chake cha Dear God kilichompa tuzo zake.

Jeremiah akaamsha simanzi ukumbini kwa kauli hii: “Katika Dear God, nilikuwa na maombi maalum kwa waliokuwa wagonjwa wetu; Sadick Juma Kilowoko (Sajuki) na Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude.’ Niliwaombea kwa Mungu kuonesha navyowapenda, lakini Mungu kawapenda zaidi.”

Jeremiah akawataka Watanzania kupendana kila mmoja kwa nafasi yake, ambapo yeye atawaenzi Sajuki na Bi Kidude aliowaombea katika wimbo huo, pamoja na ‘msela wake’ Ngwea kwa kuhakikisha anafanya kilicho bora kila mwaka. Akamaliza kwa kumtakia uponaji mwema na wa haraka, Rita Poulsen ‘Madam Rita.’

“Amenitoa mbali Madam na alipaswa kuwa hapa kushuhudia matunda haya pamoja na kupokea moja ya tuzo hizi, lakini kutokana na tukio la ajali lililompata, hayuko ukumbini hapa na sisi, namuombea kwa ‘Dear God’ apone haraka,” alisema Jeremiah na kushangiliwa na mashabiki.

Msanii Chalz Baba, aliahidi kuwalipa mashabiki waliompigia kura yeye na bendi yake ya Mashujaa kwa kuwadondoshea ‘kibao’ kipya cha ‘Ushamba Mzigo,’ huku Luiza Mbutu aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Bendi, ‘akii-dedicate’ tuzo hiyo kwa mashabiki wa Twanga Pepeta.

Washindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Raggae, kundi la Warriors From The East, wakatoa shukrani za dhati kwa waasisi wa muziki huo nchini Innocent Garinoma, Innocent Nganyagwa ‘Ras Inno’ na wengineo kwa harakati zilizoifikisha reggae mahali ilipo sasa.

Fred Maliki ‘Mkoloni’ aliyepanda jukwaani kupokea tuzo ya Wimbo Bora wa wa RnB kwa niaba ya Rama Dee aliyeshinda kupitia kibao Kuwa na Subira alichowashirikisha Mapacha, alisema nyakati za ‘vinega kuwa busy’ kikazi unaendelea kutokana na vita dhidi ya wanyonyaji kushika kasi

MPANGO WA CRISTIANO RONALDO KUREJEA ENLAND WA ONEKANA


cristiano ronaldo



MPANGO wa Cristiano Ronaldo kurejea Ligi Kuu ya England sasa uhai tena baada ya mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 80 kukanuisha taarifa za kusaini Mkataba mpya Real Madrid.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alisema mapema wiki hii kwamba alikuwa anajiamini mchezaji huyo atasaini Mkataba wa kuendelea kuichezea Real, akisema: "Lengo langu, lengo la Cristiano, na lengo la mashabiki wote wa Real Madrid ni kwamba anaendelea kucheza hapa kwa miaka mingi ijayo.’
Pamoja na hayo, akitumia ukurasa wake wa Facebook na akaunti yake ya Twitter, Ronaldo, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa, alisema: "Habari zote kuhusu kusaini kwangu Mkataba mpya Real Madrid ni uzushi,".
Dhahiri klabu yoyote duniani ingetaka kunufaika na uwezo wa Ronaldo baada ya kuzitumikia United na Madrid.
Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo unamalizika mwaka 2015, lakini amegoma kusaini mpya, Madrid haitakuwa na chaguo lingine zaidi ya kumuuza, ingawa ameunfga mabao mengi kupita kiasi,146 katika mechi 135.
Monaco ilikuwa inaaminika kujiandaa kutoa Pauni Milioni 85 na kumshawishi kwa mshahara babu kubwa ajiunge nao, lakini Ronaldo anaweza kuchagua kurejea Manchester, ambako ameacha kumbukumbu.

Alex Ferguson alikuwa anafikiriwa kuchangia kwa kiasi kikubwa Ronaldo kutorejea katika klabu hiyo, lakini anaweza kuwa na nia ya kwenda katika klabu hiyo ambayo ilimjenga na kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa dunian Chanzo na mjengwa.

Ziara ya Rais Obama yazidi kuwatia kiwewe wasomi

OBAMA1 9714d


Rais wa Marekani, Barack Obama

Ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama bado imeendelea kuwatia kiwewe Watanzania wakiwamo wasomi na wanasiasa.

Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alisisitiza kwamba Rais huyo anakuja nchini kuchunguza masuala ya madini hususan urani.

Lakini nao wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamepata hofu wakisema wana wasiwasi Tanzania itakachofaidika kwa ziara hiyo. Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, Mhadhiri wa Kitengo cha Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma, Sabatto Nyamsenda alisema hofu kubwa iliyopo inatokana na ubovu wa sera za Serikali katika masuala ya uwekezaji.

Nyamsenda aliongeza kuwa viongozi wa Serikali wamesharidhia uporaji wa rasilimali zake kupitia sera na mikataba mibovu isiyomnufaisha Mtanzania.

Profesa Robert Mabele kutoka kitengo cha uchumi chuoni hapo alisema pamoja na uhusiano ambayo Rais Kikwete amejitahidi kuujenga miongoni mwa nchi kubwa duniani, lakini hatuwezi kufaidika endapo hatutakuwa na sera nzuri za uwekezaji. Dk Jehovaness Aikaeli wa kitengo cha uchumi chuoni hapo alisema ujio wa rais huyo hautaweza kuleta mabadiliko yoyote kama inavyodhaniwa na Watanzania wengi.

Maoni hayo yanatolewa wakati juzi Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alitaja sababu za Obama kuja Tanzania kwamba ni kutokana na sifa nzuri za Tanzania. Sifa hizo zilizomvuta Rais Obama ni utawala bora, demokrasia na mazingira bora ya uwekezaji yanayosabisha kukua kwa uchumi.

Balozi wa Marekani alisema Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani, utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. ‘‘Rais Obama anakuja kuunga mkono juhudi za Watanzania katika kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na pia amevutiwa na ukuaji wa uchum

Friday 7 June 2013

STARS YAAHIDI KUFANYA KWELI KATIKA MCHEZO WAO DHIDI YA MOROCCO





Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen na Nahodha Juma Kaseja wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Pullman ilikoyo Marrakech, Morocco. Stars inashuka Jumamosikupambana na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa kufuvu kucheza fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. (Na Mpiga Picha wetu)




MARRKECH Morocco


Huku Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi) dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia, Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.


Kocha huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.


“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.


Alisema suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars, inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.


Alisema Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.


“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika mechi hii,” alisema.


Poulsena alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.


“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.


Naye nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya kuelekea Marrakech.


“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara nyingine kwa kushinda mechi hiyo.


“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.
Stars iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na Gambia 1.


Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania.


Baada ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu.

TIMU YA ARSENAL YAZIDI KUTUPA KARATA ZAKE KWA FELLAINI NA ROONEY. HUKU WENGER AKIANDAA KITITA CHA £70m


Huko London, upo uvumi mzito kuwa Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, huenda akachukuliwa na Arsenal ambao inadaiwa wako tayari kulipa Pauni Milioni 24 ambalo ndio Dau lililopo kwenye Mkataba wa Mbelgiji huyo ikiwa anataka kuvunja Mkataba na Everton. Hapo hapo uvumi mwingine unahusishwa pia na mchezaji wa United Rooney kuhamia klabu ya Gunners.

Ingawa imedaiwa sana kuwa Fellaini atamfuata aliekuwa Meneja wake huko Everton, David Moyes, ambae sasa yupo Manchester United, lakini uvumi huo wa Kiungo huyo kwenda Arsenal unadai kuwa Old Trafford inasita kumchukua hasa kwa sababu ya staili yake ya uchezaji iko tofauti na ile ya Klabu hiyo ingawa pia hilo hilo linaweza kusemwa kwa staili ya Arsenal.

Paris Saint-Germain baada ya kumkosa Radamel Falcao aliyekimbilia Monaco masikio na macho yao wameyaelekezea kwa Rooney pia na wako tayari kulipa kiasi cha £300k kwa wiki na tayari yupo kwenye tageti zao tangu siku nyingi imefahamika.