Tuesday 28 May 2013

HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA UZINDUZI WA SHINDANO LA BIG BROTHER THE CHASE

Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya kamera yetu.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.

Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg jana usiku. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

Mwakilishi kutoka Tanzania Ammy Nando akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show. Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.

Burudani zikiendelea.

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.

Mwakilishi wa Tanzania Feza Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.

Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi jana jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Feza Kessy mshiriki kutoka Tanzania.

Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo

No comments:

Post a Comment