Tuesday 2 July 2013

HAWA NDIO WACHEZAJI WATANO WANAO WAKILISHA AFRIKA KWA KUCHEZA SOKA NA KULIPWA KIASI KIKUBWA CHA PESA


Kutoka katika orodha iliyotolea na Forbes kuonyesha wanamichezo matajiri zaidi duniani ikiwa na wanamichezo kama vile Tiger Woods kama mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani - dola milioni 78.1 kwa mwaka, akifuatiwa na mcheza Tennis Roger Federer katika nafasi ya pili na Kobe Bryant katika nafasi ya tatu, Na sasa pia imefahamika ni wanasoka gani kutoka Afrika ambao wanalipwa
Hii ndiyo ile orodha iliyotolewa na Forbes hivi karibuni kuonyesha wasakata kabumbu kutoka Afrika ambao wanavuna mulla ama pesa ndefu zaidi katika kazi yao hii kutoka katika clabu mbalimbali wanazochezea.
Kwa kuanzia, katika list hii, wa kwanza kabisa ni mkali Yaya Toure, Raia wa Ivory Coast ambaye anacheza soka katika clabu ya Machester City, Kwa mwaka anaingiza Dola milioni 18.2, na mshahara wake wa wiki ni dola 320000 ambayo nnje ya bonus na allowance nyingine.




Yaya Toure
Katika nafasi ya pili yupo Samuel Eto’o kutoka Cameroon, Staa huyu anakipiga katika Clabu ya Anzhi kwa sasa, na mshahara wake kwa mwaka ni dola milioni 13.4, kwa wiki mshahara wake ni dola 300,000.



Eto'o

Wa tatu ni Didier Drogba wa Ivory Coast, kwa sasa yupo na clabu ya Galatasaray na mshahara wake kwa mwaka ni dola milioni 12.9, mpunga anaochukua kwa wiki ni dola 185,000 na pia nnje ya soka huyu ni star ambaye ana deals mbalimbali za matangazo na kampuni kama Pepsi, Nike, Samsung na Mtandao wa Orange Ufaransa.




Drogba

Mwingine ni Seydou Keita wa Mali ambaye anasakata kabumbu na clabu ya Dalian Aerbin, Mshahara wake kwa mwaka ni dola milioni 12.



Keita
Anayefuatia ni Emmanuel Adebayor kutoka Togo, Mshahara wake kwa mwaka ni dola Milioni 10, Mshahara wake kwa wiki ni dola 220,000, mbali na soka pia mchezaji huyu ana deals kadhaa za matangazo ambazo zinamuongezea mulla.


Adebayor

Tazama hichi kitu Justin Bieber alichoamua kulifanya gari lake ili tu likae 'kijanja' kama yeye alivyo vaa

Hili ndilo tukio lingine ambalo limemrudisha Mwanamuziki Justin Bieber kwenye Headlines tena, This tym round, ikiwa ni kutokana na kitendo chake cha kuamua kutoa kiasi cha paundi 125,000, ambazo ni zaidi ya shilingi 309,000,000 kwaajili ya kubadilisha rangi ya gari yake.

Bieber ameamua kuliweka gari hili rangi sawasawa na na muonekano wa 
chui, na habari za uhakika kutoka ndani ya team ya msanii huyu zinasema 
kuwa, Staa huyu aliamua kufanya  mchongo huu ili kuwezesha gari yake 
ku-match na mtoko wake wa 'kichui-chui' aliokuwa amejipanga kushine nao 
kwa siku moja.
Hivi ndio gari ya staa huyu inavyoonekana baada ya kufanyiwa mabadiliko.

RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA AMEREJEA MAREKANI LEO




Gari lililombeba Rais Obama likielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kumaliza ziara yake.



Rais Obama na mkewe michelle Obama wakipunga mikono kbla ya kuanza safari








Gari lililombeba Rais Obama likielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kumaliza ziara yake.

Msafala wa Rais obama ukipita maeneo ya buguruni kuelekea uwanja wa ndege

Sunday 23 June 2013

kocha wa arsenal ajitosa rasmi kumuwania mshambuliaji wa manchester united wayne rooney





Wayne Rooney



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
KLABU ya Arsenal baada ya kumalizana kwa dau la Pauni Milioni 22 na Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid, sasa inahamishia nguvu zake kwa mshambuliaji wa Manchester United, anayeuzwa Pauni Milioni 20, Wayne Rooney - huku kocha Arsene Wenger akiwa amedhamiria kuendelea kumtumia katika nafasi ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Muargentina huyo.

Higuain ni mchezaji ambaye Arsenal sasa wana uhakika wa kumnasa, huku Carlo Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao wa Hispania, akitarajiwa kutua leo kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.

Lakini katika uhamisho huo wa Rooney, Arsenal italazimika kumlipa mshahara wake wa Pauni 220,000 kwa wiki, ambao ni mkubwa mno kulingana na tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu 'bakhili'.
Wenger haoni kama Rooney ni mshambuliaji wa kati, lakini kama kiunganishi, baina ya kiungo na Higuain — nafasi ambayo mchezaji mwenyewe amesema inamfaa
Lakini Chelsea pia inamtaka Rooney na kocha mpya wa United, David Moyes anatarajiwa kukutana na Rooney wiki mbili zijazo, hivyo uwezekano wa yeye kujiunga na klabu hiyo ya London bado mdogo.
United haitataka kumuuza Rooney kwa Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa washindani wao wakuu katika mbio za ubingwa na matumaini ya mchezaji huyo yanabakia katika kikao chake na Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo mpya mzuri Old Trafford, hususan baada ya klabu kusema hajawahi kuomba kuondoka United.
Hilo ni suala lililotokana na wasiwasi wa Rooney juu ya uhusiano wake na mashabiki wa United. Rooney anatarajia kikao kama alichowahi kufanya na kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita, cha binafasi kujadili mustakabali wake katika klabu. Arsenal imetenga bajeti ya kutosha kupambana katoka soko la usajili, lakini tatizo ni kwamba wataweza kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa sababu ni wenye kiu ya mataji, vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo vimekuwa adimu

Brazil yaitwanga 2-1 Italia, zatinga nusu fainali kombe la mabara




Neyman akishangilia bao



Neyman akifunga bao







Javier Hernandez amefunga mawili dhidi ya Japan

MABAO ya Dante dakika ya 45, Neymar 55 na mawili ya Fred dakika za 66 na 88 yameipa Brazil ushindi waliostahili wa 4-2 dhidi a Italia usiku wa kuamkia leo na kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mabara ikishinda mechi zote katika Kundi A.

Italia ilipata mabao yake kupitia kwa Giaccherini dakika ya 51 na Chiellini dakika ya 71.

Kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz/Dante dk33, Marcelo, Gustavo, Hernanes, Hulk/Fernando dk76, Oscar, Neymar/Bernard dk68 na Fred.

Italia: Buffon, Abate/Maggio dk30, Bonucci, De Sciglio, Chiellini, Candreva, Aquilani, Marchisio, Montolivo/Giaccherini dk26, Diamanti/El Shaarawy dk71 na Balotelli.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Javier Hernandez alifunga mabao mawli na kukosa penalti Mexico ikiifunga Japan 2-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A. Bao la Japan lilifungwa na Shinji Okazaki na sasa Brazil inaungana na Italia kusonga Nusu Fainali.

Saturday 22 June 2013

IMEVUJA, MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA





TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa

HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA SHOW YA MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGA(NEW MSASANI DSM)



Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam.

Chid Benz
Fukuda akichana mistari

Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.


Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi.
Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.


Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza





Afande Sele akipagawisha mashabiki.

MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA CROATIA AFARIKI DUNIA UWANJANI



Alen Pamic aliyelala, akipatiwa huduma ya kwanza na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni kutokana na matatizo ya moyo.
ALEN PAMIC

ZAGREB, Croatia
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo
NYOTA wa soka la kulipwa raia wa Croatia, Alen Pamic ameanguka uwanjani na kufariki dunia wakati wa mechi ndogo isiyo ya kimashindano, gazeti la kila siku la Vecernji List limesema katika toleo lake mtandaoni la leo Jumamosi.
Taarifa hiyo imeripotiwa kwa ufupi, huku ikiwa haina maelezo zaidi kuhusiana na kifo cha Pamic aliyekufa akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic, aliyekuwa akichezea klabu ya NK Istra 1961 katika ligi ya daraja la juu zaidi nchini hapa, alikuwa na historia ya matatizo ya moyo, ambayo yalimwangusha dimbani mara tatu kabla ya tukio hilo lililochukua uhai wake.
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo.
Pamic aliyekuwa kiungo mahiri dimbani, aliutumia msimu mmoja wa 2010/11 kuchezea klabu ya Standard Liege ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, lakini klabu hiyo ikamtema muda mfupi baada ya kupata shambulio la moyo na kuzimia akiwa mazoezini, gazeti la Vecernji limesema katika taarifa yake.
Pamic ni mtoto wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Croatia, Igor Pamic, ambaye kwa sasa anainoa klabu ya NK Istra 1961 aliyokuwa akiichezea marehemu

HUU NDIO UJIO MPYA WA AMINI

AMINI

BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Ni wewe’, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’ anajipanga kuachia video ya kibao chake cha ‘Sipo nae’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaama, Amini alisema anamshukuru mungu kazi hiyo imefanya vizuri na anaamini itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya kibao hicho.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika studio ijulikanayo kwa jina la Shany chini ya mtengenezaji mahiri Mr. T ambaye anauhakika amemtendea haki katika kazi hiyo.
“Mtayarishaji wangu namuamini sana, hivyo najua wadau wengine wataupenda wimbo kulingana na vionjo ambavyo amevitumia mbali na ujumbe uliopo katika kazi hiyo.” alisema Amini.
Pia aliwaomba wadau na mashabiki wa muziki nchini kumpa sapoti katika kazi zake na wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Amini alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Robo saa’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga

ROONEY KUVUTWA SHATI KATIKA TIMU YA REAL MADRID

WYNE ROONEY



KOCHA mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atafanya harakati za kumsajili Wayne Rooney majira haya ya joto kama mshambuliaji huyo asiye na furaha atashindwa kumaliza tofauti zake na Manchester United.

Rooney anapenda zaidi kuungana na Jose Mourinho pale Chelsea ikiwa atamaliza miaka yake tisa ya kuishi United, lakini Madrid itakuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa ataondoka.

Klabu zote zina uwezo sana tu wa kulipa Pauni Milioni 30 za ada ya uhamisho wake na kumlipa mchezaji mwenyewe mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Ancelotti anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho Jumatatu na atakabidhiwa orodha ya wachezaji wanaotakiwa, wakiwemo Rooney, Gareth Bale, Edinson Cavani na Luis Suarez. Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake, atakuwa na mazungumzo na kocha mpya wa United, David Moyes baada ya wote kurejea kutoka mapumziko

HII HAPA HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA LA(1)





FUFA WORLD CUP HISTORY



WAKATI vugugu la kuelekea kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil likipamba moto, ni vema

tukaipitia historia ya mchezo wa kandanda ili, kwetu wapenzi wa mchezo huo, kujikumbusha historia yake.

Naam, mchezo wa kandanda una historia ndefu. Mwaka 1863 ndipo pale kandanda ya mpangilio ilipoona mwanga wa dunia. Hii ni baada ya nchi ya Uingereza kuutengenezea
mchezo huo sheria , kanuni na taratibu za kuucheza. Kabla ya hapo, kandanda
ulikuwa ni mchezo uliochezwa bila mpangilio maalum. Kulikuwa hakuna
sheria wala kanuni zilizowekwa juu ya mchezo huo.

Ni kwa sababu hii, Uingereza hadi leo hii inajiona kuwa ni “Mama wa Kandanda”. Matukio kadhaa ya


kihistoria ya mchezo huo yameonyesha ni jinsi gani Uingereza , kwa kujiona kuwa wao ndio waanzilishi wa kandanda duniani, wamekuwa wakionyesha majigambo ya wazi na wakati mwingine kuzuia kwa makusudi juhudi za wengine katika kufikiri namna nzuri ya kuuendeleza mchezo huo, mchezo ambao Waingereza wanaamini kuwa ni wao.

Hakuna ajabu baada ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mara ya kwanza mwaka 1966,
Uingereza ilionyesha azma yake ya kuandaa fainali za mchezo huo
kwa mwaka 2018. Hata hivyo, Qatar ndio iliyopata bahati hiyo.

Ikumbukwe, kuwa mwaka 2012 Uingereza iliandaa michezo ya
olimpiki kwa mataifa ya dunia. Kama wangepewa nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia miaka sita baada ya 2012, yaani, 2018, basi, Waingereza wangependa waitangaze nchi yao, kama taifa ambalo, katika kipindi cha mwongo mmoja ( miaka kumi) limeweza kupata
mafanikio makubwa na ya kihistoria ya kimichezo kwa kuwa mwenyeji wa matukio
makubwa mawili ya kimichezo duniani; Olimpiki na Fainali za Kombe la Dunia.
Kwamba Uingereza ni taifa kubwa.

Siku zote, Uingereza inajivunia historia ya kandanda kuwa upande wao. Itakumbukwa, kuwa ilikuwa ni mwezi Oktoba ya tarehe 26 mwaka 1863 pale shirikisho la kandanda nchini Uingereza (FA) lilipoanzishwa rasmi jijini London. Miaka 17 iliyofuata hata Scotland, Wales. Ireland nazo zikaanzisha mashirikisho yao ya soka.

Denmark ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Uingereza kuanzisha shirikisho lake la soka. Ilikuwa ni mwaka 1889. Lakini FIFA, shirikisho la soka duniani lilipoanzishwa rasmi mwaka 1904, liliundwa bila kuishirikisha Uingereza. Hii ilitokana na Uingereza kutokutuma mwakilishi wake kwenye majadiliano ya kuanzishwa kwa FIFA.

Kilichopelekea hilo ni dharu ya Waingereza ambao waliamini, kuwa
FIFA haikiuwa na lolote la kuchangia katika soka ukiondoa Waingereza wenyewe
walioasisi mchezo huo. Kwa namna fulani, ni hapa tunaweza pia kuyaona majigambo ya Waingereza katika kandanda.

Kwa vile Uingereza inaundwa na visiwa, kuna utani, kuwa hii ni hulka ya watu
waishio visiwani; kuwa hawaoni kingine mbali ya maji yaliyo mbele yao,
hujiona kuwa wao ni kila kitu.Uingereza waliendelea kuigomea FIFA na kutojihusisha nayo hadi mwaka 1924.


Nchi zilizotuma wajumbe waliohusika na kuunda FIFA ni kama zifuatazo;
Ubelgiji, Ufaransa, Hispania, Uholanzi, Denmark na Sweden. Vinara
waliopelekea kuundwa kwa FIFA ni matajiri wawili wakubwa kwa wakati huo;
Mholanzi Hirschman na Mfaransa Robert Guerin.

Kitendo cha Uingereza cha kujitazama yenyewe tu na kuibuka kwa
Vita Kuu Ya Kwanza ya Dunia kulipelekea mipango ya FIFA kuanzisha michezo ya
Kombe La Dunia kwa mara ya kwanza kuahirishwa na kusogezwa mbele. Na hata
vita vilipomalizika, Uingereza ilikataa katakata kuruhusu timu yake ya taifa
pamoja na washirika wao katika vita kukutana na kucheza na timu za mataifa
yaliyokuwa adui zao katika vita.

Hata hivyo, pamoja na Uingereza kujiunga na FIFA mwaka 1924, bado katika Fainali za kwanza za Kombe la Dunia zilizoandaliwa na FIFA mwaka 1930, Uingereza haikushiriki. Walisusa tena.

Je, ni kwanini Waingereza walisusa kucheza fainali za kwanza za
Kombe la Dunia? Je, jeuri na majigambo haya ya Waingereza ni sawa na mbio za
sakafuni ambazo huishia ukutani? Ni nini ilikuwa hatma ya msuguano huu kati
ya FIFA na Waingereza? Endelea kufuatilia simulizi hii ya kombe la dunia

0752887944 mwendaa lucas



Friday 14 June 2013

Bajeti : Ushuru wapiga hodi kwa watumiaji fedha kwa simu,ahueni kwa wamiliki wa bodaboda

 Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akiingia bungeni Dodoma jana kusoma hotuba ya Bajeti. Picha na Fidelis Felix
Dar na Dodoma:  
Serikali jana ilitangaza Bajeti yake kuu kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambayo inaashiria machungu kutokana na ongezeko la kodi na ushuru katika baadhi ya bidhaa, zikiwamo mafuta, soda, vinywaji vikali pamoja na leseni za magari.

Akisoma bajeti hiyo bungeni jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa pia alitangaza kuanzisha kodi na ushuru katika huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia simu za mkononi, ikiwamo kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha.

“Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 14.5 kwenye huduma zote (all mobile phone services) za simu za kiganjani/mkononi badala ya muda wa maongezi tu (airtime alone),” alisema Dk Mgimwa na kuongeza: “Katika ushuru huu, asilimia 2.5 zitatumika kugharimia elimu nchini.”
Kutokana na hali hiyo, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk Oswald Mashindano amelaumu kile alichokiita kuwa ukubwa wa kodi hasa kwa wasio na kipato kikubwa ili kufidia uendeshaji wa Serikali.

“Kama kawaida kutakuwa na ongezeko la mapato ya Serikali kutoka katika vyanzo vyake hasa ukusanyaji wa kodi. Inamaanisha kuwa kutakuwa na mzigo mkubwa kwa walipakodi hasa kundi la wenye kipato kidogo.

“Tofauti na nchi zilizoendelea ambazo wenye mitaji mikubwa ndiyo wanaobanwa kulipa kodi zaidi, nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwamo, kuna udhaifu mkubwa wa kukusanya kodi,” alisema Dk Mashindano.
Mafuta na magari

Waziri Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itapandisha ushuru wa mafuta ya dizeli kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 kwa lita, likiwa ni ongezeko la shilingi 2.

“Tumeongeza Sh2 tu kwa kuwa tunatambua tukiongeza ushuru mkubwa kwa magari makubwa ambayo yanatoa huduma kwa jamii, tutawaumiza wananchi,” alisema Dk Mgimwa.

Kadhalika, ushuru wa mafuta ya petroli umeongezwa kwa Sh61, kutoka Sh339 kwa lita hadi Sh400. Hata hivyo, imeongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa lita, sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita na wakati huohuo mafuta hayo yakiongezewa Sh50 kwa kila lita, fedha zitakazotumika kuchangia mfuko wa kusambaza umeme vijijini.

Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), umeongezewa kiasi cha Sh186.9 bilioni ambazo awali, hazikuwa zimetengwa baada ya Serikali kukubaliana na mapendekezo ya Bunge kupitia Kamati yake ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Serikali pia imepandisha viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari. Magari yenye ujazo wa injini yenye ukubwa wa kati ya cc 501 na 1500 yatatozwa Sh150,000 kutoka Sh100,000 za sasa.
Magari yenye ujazo wa cc 1501 hadi  2500 kiwango chake kimeongezeka kutoka Sh150,000 hadi Sh200,000 wakati magari yenye ujazo wa injini zaidi ya cc 2501 yatatozwa Sh250,000 kutoka kiwango cha sasa ambacho ni Sh200,000.

Hata hivyo, uamuzi huo hautazigusa bajaji na pikipiki (maarufu kama bodaboda) kwani Dk Mgimwa alisema vyombo ambavyo injini zake zina ujazo chini ya cc 501, ambavyo havitatozwa ada ya leseni. Ushuru pia umeongezwa kwenye magari yasiyokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25. Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari  chakavu  ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.

Pombe na Sigara

Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali na sigara. Vimeongezwa kodi kwa asilimia 10.
Ongezeko la kodi kwa kipimo cha lita moja ni kwa vinywaji vikali ambayo imepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631, sawa na ongezeko la Sh239, bia inayotengenezwa kwa nafaka za nchini ambayo haijaoteshwa, imepanda kutoka Sh310 hadi Sh341, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita wakati bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 hadi Sh578 sawa na ongezeko la Sh51.

Vinywaji baridi vimepanda kutoka Sh83 kwa lita hadi Sh91 sawa na ongezeko la Sh8 kwa lita.

Sigara zenye kichungi na zinazozalishwa nchini zimepanda kwa asilimia 75, kutoka Sh19,410 hadi Sh21, 351 kwa sigara 1,000 sawa na ongezeko la Sh1.94 na senti 94 kwa sigara moja.
Mabadiliko ya Sheria

Ili kutekeleza uamuzi wa kuongeza ushuru na kodi, Dk Mgimwa amependekeza kufanya maboresho ya sheria mbalimbali za kodi ambazo ni za; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Kodi ya Mapato, Ushuru wa Bidhaa, Ushuru wa Mafuta, Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Sheria ya Usalama Barabarani. Nyingine ni Sheria za; Petroli (Petroleum Act), Uwekezaji Tanzania, Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na marekebisho mengine madogomadogo katika baadhi ya sheria za kodi.

Dk Mgimwa alisema mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji yanalenga kutoza asilimia 25 ya ushuru wa forodha unaopaswa kutozwa kwenye bidhaa zinazotambulika kama “Deemed Capital Goods” (yaani kutoa msamaha wa kodi wa asilimia 75 kwenye bidhaa hizo badala ya asilimia 90 za sasa) na kuondoa baadhi ya bidhaa kwenye orodha ya kupata msamaha.

“Bidhaa hizo ni zile ambazo hazina uasilia wa kuwa bidhaa za mtaji kama vile vifaa vya ofisi, samani, sukari, vinywaji (viburudisho), bidhaa za mafuta ya petroli, magari madogo (Non Utility Motor Vehicles), viyoyozi, majokofu, na vifaa vya kielektroniki, mashuka, vijiko, vikombe nk,” alisema waziri huyo. Alisema marekebisho hayo pia yanalenga kupunguza misamaha ya kodi na kubakiza misamaha yenye tija na yenye kuchochea uwekezaji mkubwa katika sekta za uchumi za kimkakati, hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Alisema pato la taifa linatarajiwa kukua kutoka asilimia 7.0 mwaka 2013 hadi asilimia 7.2 mwaka 2014 na wakati huohuo, bei zikitarajiwa kubaki kwenye viwango vya tarakimu moja na mfumuko wa bei kushuka hadi asilimia 6.0 Juni 2014.
Kuhusu akiba ya fedha za kigeni, Dk Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali itajitahidi kuwa na akiba itakayoweza kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Alisema jitihada zitafanywa ili kupunguza tofauti ya viwango vya riba vya kuweka na kukopa na kuimarisha thamani ya shilingi na kuwa na kiwango imara cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

Mbowe, wabunge

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe alisema: “Bajeti ya mwaka huu haina jipya” kwani Serikali imeendelea kupandisha kodi katika bidhaa zilizozoeleka badala ya kusimamia kodi kwenye rasilimali za nchi.
“Bajeti hii inaonyesha Serikali ilivyokosa ubunifu wa vyanzo vya mapato, kila mwaka wanapandisha kodi kwenye bia, sigara, magari na mafuta,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia alisema sheria ya ununuzi ikirekebishwa kama alivyoahidi Waziri Mgimwa itasaidia kupunguza gharama ya bidhaa mbalimbali.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema kuongezwa kwa fedha za mfuko wa vijana ni ukombozi kwa kuwa miaka mingi kilio hicho hakikusikika.

“Tunaona sasa Serikali imekuwa sikivu kwa kuwa kwa muda mrefu tuliomba lakini hatukupewa,” alisema baada ya Serikali kuongeza Sh3 bilioni kwa ajili ya mfuko