Monday 3 June 2013

MAELFU WA ANDAMANA ADDIS ABABA



Maelfu ya waandamanaji wameandamana katika barabara za mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakidai waandishi wa habari na wanaharakati walioko kizuizini wafunguliwe.

Waandishi wa habari wanasema ni nadra kuonesha upinzani wa namna hiyo kwa chama tawala ambacho kinadhibiti shughuli za jamii sawasawa.

Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema serikali imetumia sheria za kupambana na ugaidi ili kuwafunga waandishi wa habari.



Waandamanaji- wengi kutoka upinzani - walipiga kelele kudai uhuru na haki. Haya ni maandamano ya kwanza tangu mwaka wa 2005 ambapo mamia ya waandamanaji waliuliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguziA

No comments:

Post a Comment