Saturday 22 June 2013

HII HAPA HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA LA(1)





FUFA WORLD CUP HISTORY



WAKATI vugugu la kuelekea kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil likipamba moto, ni vema

tukaipitia historia ya mchezo wa kandanda ili, kwetu wapenzi wa mchezo huo, kujikumbusha historia yake.

Naam, mchezo wa kandanda una historia ndefu. Mwaka 1863 ndipo pale kandanda ya mpangilio ilipoona mwanga wa dunia. Hii ni baada ya nchi ya Uingereza kuutengenezea
mchezo huo sheria , kanuni na taratibu za kuucheza. Kabla ya hapo, kandanda
ulikuwa ni mchezo uliochezwa bila mpangilio maalum. Kulikuwa hakuna
sheria wala kanuni zilizowekwa juu ya mchezo huo.

Ni kwa sababu hii, Uingereza hadi leo hii inajiona kuwa ni “Mama wa Kandanda”. Matukio kadhaa ya


kihistoria ya mchezo huo yameonyesha ni jinsi gani Uingereza , kwa kujiona kuwa wao ndio waanzilishi wa kandanda duniani, wamekuwa wakionyesha majigambo ya wazi na wakati mwingine kuzuia kwa makusudi juhudi za wengine katika kufikiri namna nzuri ya kuuendeleza mchezo huo, mchezo ambao Waingereza wanaamini kuwa ni wao.

Hakuna ajabu baada ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mara ya kwanza mwaka 1966,
Uingereza ilionyesha azma yake ya kuandaa fainali za mchezo huo
kwa mwaka 2018. Hata hivyo, Qatar ndio iliyopata bahati hiyo.

Ikumbukwe, kuwa mwaka 2012 Uingereza iliandaa michezo ya
olimpiki kwa mataifa ya dunia. Kama wangepewa nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia miaka sita baada ya 2012, yaani, 2018, basi, Waingereza wangependa waitangaze nchi yao, kama taifa ambalo, katika kipindi cha mwongo mmoja ( miaka kumi) limeweza kupata
mafanikio makubwa na ya kihistoria ya kimichezo kwa kuwa mwenyeji wa matukio
makubwa mawili ya kimichezo duniani; Olimpiki na Fainali za Kombe la Dunia.
Kwamba Uingereza ni taifa kubwa.

Siku zote, Uingereza inajivunia historia ya kandanda kuwa upande wao. Itakumbukwa, kuwa ilikuwa ni mwezi Oktoba ya tarehe 26 mwaka 1863 pale shirikisho la kandanda nchini Uingereza (FA) lilipoanzishwa rasmi jijini London. Miaka 17 iliyofuata hata Scotland, Wales. Ireland nazo zikaanzisha mashirikisho yao ya soka.

Denmark ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Uingereza kuanzisha shirikisho lake la soka. Ilikuwa ni mwaka 1889. Lakini FIFA, shirikisho la soka duniani lilipoanzishwa rasmi mwaka 1904, liliundwa bila kuishirikisha Uingereza. Hii ilitokana na Uingereza kutokutuma mwakilishi wake kwenye majadiliano ya kuanzishwa kwa FIFA.

Kilichopelekea hilo ni dharu ya Waingereza ambao waliamini, kuwa
FIFA haikiuwa na lolote la kuchangia katika soka ukiondoa Waingereza wenyewe
walioasisi mchezo huo. Kwa namna fulani, ni hapa tunaweza pia kuyaona majigambo ya Waingereza katika kandanda.

Kwa vile Uingereza inaundwa na visiwa, kuna utani, kuwa hii ni hulka ya watu
waishio visiwani; kuwa hawaoni kingine mbali ya maji yaliyo mbele yao,
hujiona kuwa wao ni kila kitu.Uingereza waliendelea kuigomea FIFA na kutojihusisha nayo hadi mwaka 1924.


Nchi zilizotuma wajumbe waliohusika na kuunda FIFA ni kama zifuatazo;
Ubelgiji, Ufaransa, Hispania, Uholanzi, Denmark na Sweden. Vinara
waliopelekea kuundwa kwa FIFA ni matajiri wawili wakubwa kwa wakati huo;
Mholanzi Hirschman na Mfaransa Robert Guerin.

Kitendo cha Uingereza cha kujitazama yenyewe tu na kuibuka kwa
Vita Kuu Ya Kwanza ya Dunia kulipelekea mipango ya FIFA kuanzisha michezo ya
Kombe La Dunia kwa mara ya kwanza kuahirishwa na kusogezwa mbele. Na hata
vita vilipomalizika, Uingereza ilikataa katakata kuruhusu timu yake ya taifa
pamoja na washirika wao katika vita kukutana na kucheza na timu za mataifa
yaliyokuwa adui zao katika vita.

Hata hivyo, pamoja na Uingereza kujiunga na FIFA mwaka 1924, bado katika Fainali za kwanza za Kombe la Dunia zilizoandaliwa na FIFA mwaka 1930, Uingereza haikushiriki. Walisusa tena.

Je, ni kwanini Waingereza walisusa kucheza fainali za kwanza za
Kombe la Dunia? Je, jeuri na majigambo haya ya Waingereza ni sawa na mbio za
sakafuni ambazo huishia ukutani? Ni nini ilikuwa hatma ya msuguano huu kati
ya FIFA na Waingereza? Endelea kufuatilia simulizi hii ya kombe la dunia

0752887944 mwendaa lucas



No comments:

Post a Comment