Monday 3 June 2013

DOTMUND YATAKA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI WA ARSENAL



LUKAS PODOLSK

KLABU ya Borussia Dortmund inataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, aliyefunga zikiwa zimesalia dakika tisa katika ushindi wa 4-2 kwa nchi yake dhidi ya Ecuador mapema wiki hii, anatakiwa na wafungwa hao wa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Podolski amefunga mabao 16 katika msimu wake wa kwanza Emirates baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 11 kutoka msimu uliopita.

Lakini Arsene Wenger anaweza kukabiliana na ushindani kumbakiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Dortmund, ambao wamempoteza Mario Gotze aliyehamia Bayern Munich. Klabu hiyo ya Ujerumani pia inahitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa Gotze na Robert Lewandowski pia anatarajiwa kuondoka

No comments:

Post a Comment